Wednesday, 25 December 2013

TANGAZO! TANGAZO! TANGAZO
Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Vyuo Vikuu Afrika Mashariki tawi la Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro,kinataraji kufanya Tamasha la siku ya Kiswahili.Tamasha hili litakuwa ni tarehe 01/01/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.
MAHALI;Ukumbi wa Mikutano wa Chuo na Baadae Uwanja wa Mpira wa Miguu.
MAMBO YATAKAYOJUMUISHWA;
  • Uzinduzi wa kitabu cha ushairi
  • Uchambuzi yakinifu wa kazi za Fasihi
  • Maghani
  • Igizo
  • Mpira wa Miguu
  • Mashindano ya kukuna nazi
  • Kuvuta kamba
  • Kukimbiza kuku
Njoo upate Elimu,njoo Uburudike   
KISWAHILI HAZINA YA AFRIKA KWA MAENDELEO ENDELEVU