Tuesday, 5 November 2013

MKUTANO WA WANAFUNZI WA KISWAHILI NA VIONGOZI WA CHAWAKAMA TAWI

Mkutano huo ulifanyika tarehe  4/11/2013 siku ya Jumatatu, katika ukumbi mpya wa mikutano uliopo chuoni hapo. Mkutano huo ulihusisha Wanafunzi wote wasomao Kiswahili kuanzia Mwaka wa Kwanza, wa Pili na mwaka waTatu, ulijikita zaidi katika kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwa pamoja na:  namna ya kujiunga na chama, faida ya kuwa mwanachama, taarifa kuhusiana na Makongamano mbalimbali yanayotaraji kufanyika ndani na nje ya nchi, sambamba na mikakati na mipango mbalimbali ya kukiendeleza chama.
Baadhi ya wanachama waliohudhuria katika Mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa Tawi wakiongozwa na Mwalimu Mlezi Bwana Hamad Abdallah, Mwenyekiti wa Tawi ndugu Adam Matimbwa, Katibu mkuu wa A.Mashariki ndugu Ahmad Jumbe, Katibu wa Tawi ndugu Abdallah Kiula na Katibu mwenezi wa Tawi ndugu Mohamed Khalfani
Wajumbe ambao ni Wanafunzi wanaosoma Kiswahili chuoni hapo, wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Viongozi wa Chawakama Tawi.
Wajumbe wa Mkutano huo
Wajumbe wa Mkutano huo wakifuatilia kwa makini Mkutano huo

No comments:

Post a Comment